Uhuru aagiza mchele kutoka Mwea ununuliwa kwa wakulima Ksh. 84
У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Rais Uhuru Kenyatta kwa siku ya pili mtawalia amezuru eneo la mlima kenya, akiwa na kapu la vinono ili kuziteka nyoyo za wenyeji huku mchakato wa bbi ukishika kasi. Kenyatta ameagiza wakulima wa mpunga walipwe shilingi 85 kwa kila kilo ya mchele, na kuzitaka taasisi za serikali kununua mchele wa humu nchini na wala si ule wa kigeni. Nao wanasiasa wanaoegemea mrengo wa naibu rais william ruto wanazidi kusukumwa, huku kenyatta akitoa ilani ya kufurushwa na kushtakiwa kwa magavana wanaodaiwa kupora mali ya umma.