Simba 2-1 Mwadui - Kombe la Shirikisho la Azam Sports
У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamefanikiwa kutinga raundi ya tano (16 bora) katika michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) baada ya kuifunga Mwadui FC mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa leo (25/01/2020) kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mwadui ndiyo waliotangulia kupata bao kupitia kwa Gerald Mathias Mdamu dakika ya 35 kabla ya Clatous Chama kusawazisha dakika ya 45+2 na Francis Kahata kupiga la pili dakika ya 85.
(ASFC - 25/01/2020)