MAGOLI: COASTAL UNION 1-2 SIMBA SC: (TPL - 17/04/2019)
У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wameendelea wimbi la ushindi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya leo kuichapa Coastal Union mabao 2-1 kwenye Dimba la Mkwakwani Jijini Tanga.
Wenyeji Coastal ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya kwanza kupitia kwa Raizin Hafidh baada ya beki wa Simba Erasto Nyoni kuchanganyana na kipa wake Aishi Manula kuchanganyana.
Dakika ya 48 Simba walipata penati baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa ndani ya 18 na kipa wa Coastal Union, penati ambayo ilifungwa na Meddie Kagere ambaye pia aliifungia Simba bao la pili dakika ya 68.
Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kujiimarisha kwenye nafasi yake ya tatu ikifikisha pointi 60 huku Coastal Union wakiwa nafasi ya nane na pointi 41.