Huyu ni Mkurugenzi wa Bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, lakini pia ni mwanasiasa mashuhuri ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaitwa Asha Baraka, ndiye aliyekuwa mgeni kwenye kipindi hiki cha Nyundo ya Baruan Muhuza cha Alhamisi ya leo Desemba 27, 2018.
Amezungumza mengi, ikiwemo kinachomfanya aitwe ‘Iron Lady’ ikiimanisha chuma katika Nyanja zote ambazo yuko hasa siasa, michezo na muziki. Nini kinachofanya watu wamkubali?
Nini siri ya mafanikio yake hadi kuwa mwanamke pekee aliyeweza kuongoza bendi ya muziki wa dansi na ikadumu kwa muda mrefu tena kwa mafaniko? Nini anachokitafuta katika michezo, kwanini alipata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ndani ya Simba na mengine mengi.
Asha pia amevunja ukimya kuhusu umiliki wa bendi hiyo, je ni bendi ya familia? Na vipi kuhusu historia yake kimuziki, na michezo? Bila kusahau maisha yake binafsi ambapo amesisitiza kuwa hataki kutumia jina la mume licha ya kutoweka wazi iwapo ana mume au la.
#NyundoYaBaruanMuhuza ni kila Alhamisi saa 1:00 usiku #AzamSports2