У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Huku watahiniwa wa mtihani wa darasa la nane kcpe wakisubiri matokeo ya kuwawezesha kujiunga na kidato cha kwanza mwakani, tohara kwa wavulana wapatao mia mbili walioko kwenye kiwango hicho katika kaunti ya Meru iliendeshwa kwa ufanisi mkubwa chini ya usimamizi wa kanisa la Methodist. Anavyoripoti Frank Otieno, tohara hapa inaashiria kuvuka na kuingia kwenye kiwango cha uwajibikaji na ndiposa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza ni sharti watahiriwe ili kujiandaa kuchukua majukumu mazito katika jamii.
Watch KTN Streaming LIVE from Kenya 24/7 on http://www.ktnkenya.tv