Gari La Mhubiri Lapatikana Na Sehemu Za Mwili Wa Binadamu, Mombasa
У вашего броузера проблема в совместимости с HTML5
Mwanamume mmoja amekamatwa jijini Mombasa akiwa na mfuko uliojaa vitu vinavyoshukiwa kuwa vipande kadhaa vya sehemu za mwili wa binadamu.
Mwanamme huyo alikiri mbele ya maafisa wa polisi kwamba bidhaa hizo zinamilikiwa na mhubiri mmoja wa kanisa fulani eneo la Magongo, Changamwe mjini Mombasa. Kisa hicho kilizua kizazaazaa pale mwanamume huyo aliyekamatwa alipagawa ghafla na kuanza kugaagaa chini kama aliyeingiwa na pepo.