DODOMA: Naibu waziri Nchi ofisi ya Waziri Mkuu , kazi, ajira na vijana, Antony Mavunde amewataka watumishi wa mfuko wa hifadhi ya jamii, PSSSF Mkoa wa Dodoma kuendelea kutoa Elimu kwa wastaafu na wafanya kazi juu ya uunganishaji wa mifiko hiyo.
Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati alipotembelea ofisi za mfuko huo ili kujionea shughuri zinazofanywa na mfuko huo, amesema watumishi wa mfuko huo wanawajibu wa kutoa Elimu kwa watumishi pamoja na wasitaafu juu ya uungwanishwaji wa mifuko hiyo.
Ili kila mtu aelewe madhumuni ya kuunganisha mifuko hiyo, vilevile amewataka kuwapa elimu waajiri juu ya michango ya wanachama, pamoja na wafanya kazi kupewa elimu juu ya michango hiyo na faida zake baada ya kustaafu.
Pia Naibu waziri Mavunde amesema pamoja na yote lengo la Serikali kuunganisha mifuko hiyo ni kupunguza matumizi na gharama ya uendeshaji wa mifuko hiyo, na kutoa huduma bora kwa wananchi, vilevile amewataka watumishi hao kutoa huduma bora na kwa wakati.
Awali Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma Meshack Bandawe alisema Ofisi hiyo inahudumia Wilaya zote za mkoa wa Dodoma na inawaajiri mia mbili na ishilini 220 na wanachama zaidi ya laki moja(100,0000), pia amesema wamepokea madai mia saba tisini na mbili (792)kutoka kwa iliyokuwa mifuko ya awali, na kati ya hayo madai mia saba kumi na saba(717) yameshughurikiwa na mengine sabini na tisa yanashughurikiwa.